Ijumaa, 3 Julai 2015

HUU HAPA UTANGULIZI WA KITABU KIPYA CHA RIWAYA CHA MWANDISHI CHIPUKIZI NDUGU. CLEMENCE JOSEPH NYONI


JINA LA RIWAYA: "NILIKUWA MWAMBA KATIKA BIASHARA YA                                                                  MADAWA YA KULEVYA NA UJAMBAZI WA KIMATAIFA"


MTUNZI/MWANDISHI: Clemence Joseph Nyoni
MHARIRI: Oswald Ngonyani
MAWASILIANO: 0766 875 334 au O767 57 32 87
BEI: Tsh. 7500/-
WACHAPISHAJI: Peramiho Printing Press 
NB: (Kwa wateja wa Jumla tuwasiliane kupitia namba tajwa za hapo kati)


       
Riwaya hii inawahusu vijana wawili mmoja aliyejiita Master na Mwingine akiitwa Doctor Bon. Master ndiye aliyeanza biashara ya madawa ya kulevya akishirikiana na  mwanamke mmoja aliye julikana kwa jina la Ester.

Lakini  baadaye Master aliweza kufanya mbinu za kumwingiza Doctor Bon katika biashara hii ya madawa ya kulevya ambaye alikuja Arusha akitokea Songea. Ndipo walipokuwa maarufu ndani ya jiji la Arusha,  baadaye walishirikiana kupoteza uhai wa Ester kutokana na kudhurumiana hivyo wakaamua kukimbilia mjini Mombasa na baadaye kuishi Tanga. Urafiki wa Doctor Bon na Master haukudumu kutokana na mambo yaliyokiuka urafiki wao.
          
Hivyo Doctor Bon akakimbilia South Africa huku Master akikimbilia Italia. Doctor alikuja kuwa maarufu  ndani ya  nchi ya South Africa alipopata marafiki wengi ndani ya nchi hiyo na kusumbua vyombo vya habari nchini humo na hata kufanikiwa kushinda kesi nyingi alizofunguliwa, lakini Master aliamua kumtafuta Doctor Bon baada ya kusikia yupo nchini humo.
           
Kutokana na usumbufu aliokuwa anaupata Doctor Bon akiwa South Africa, Doctor  Bon akaamua kukimbilia nchini  Marekani maeneo ya Los angeles na kuishi huko.Visa vya Master vilimfanya aingie matatani baada ya kupambana na kikosi cha Doctor Bon. 
   
Kitabu hiki kina visa vingi na mikasa iliyowakuta vijana hawa katika biashara ya madawa ya kulevya na ujambazi wa kimataifa.

Ili kuujua undani wake ni vema ukajipatia nakala yako mapema.............

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni