Ijumaa, 3 Julai 2015


CHUO KIKUU CHA IRINGA KESHO KINATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALII NA UTAMADUNI


Na Fredy Mgunda, Iringa

Chuo kikuu cha IRINGA ZAMANI TUMAINI kesho kinatarajiwa kuadhimisha siku ya utalii wa kitamaduni katika chuo hicho.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii mkuu wa kitengo cha utalii cha chuo hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kuwakumbusha wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.

Aidha SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha
elimu ya utalii ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja kwa moja jamii ambayo haina elimu hiyo.

“Tunaona wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni
lakini hawana wateja kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa wateja hata hivyo mama ntilie wengine hutoa huduma kwa kutofata mazingira yakiafya”.alisema SANGA

Ameongeza kuwa watanzania wengi hatuna tabia ya kuupenda utamaduni wetu au kuipenda asili yetu tunaona wananchi wengi wanapenda kuiga utamaduni wa kigeni hivyo tunatakiwa kuuenzi utamaduni wetu.

SANGA amemalizia kwa kuwataka wanachi wajitokeze siku ya
jumamosi ili kujionea vitu mbalimbali ya kitamaduni.

Kwa upande wao WANAFUNZI WA CHUO HICHO hasa wanaosomea masomo ya maliasili na utalii wamewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hao.

JIONEE PICHA ZAIDI ZA MHADHILI WA CHUO HICHO BW. JIMSON SANGA


                   MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA 



                 Baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani Tumaini




                                     Majengo mengineyo ya Chuo hicho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni