CHAMA KISICHOTAMBULIKA KISHERIA CHAENDESHA LIGI YA SOKA HUKO MPITIMBI NA KUWAACHA WAKAZI WA KATA HIYO WAKIBAKI BABAIKONI
Na Andrew Mhaiki, wa Mwanaperamiho blog.
BAADHI ya wadau wa soka kutoka vijiji vya kata ya Mpitimbi huko Songea vijijini wamelalamika kuwa viongozi wao wa Serikali ya kata hiyo wamekuwa wakiendesha mashindano ya soka kinyume cha sheria kwa madai kuwa wao wanafuata miongozo, taratibu, sheria na kanuni za chama cha soka Tanzania (FAT)
ambayo imepitwa na wakati badala ya ya Shirikisho la
mpira wa miguu Tanzania(TFF)
Walisema pamoja na viongozi wao wa Serikali ya kata hiyo kudai wanafuata miongozo, taratibu, sheria na kanuni ambazo zilizowekwa na chama chao cha FAT, bado kata hiyo
ya Mpitimbi kwa upande wa soka inasimamiwa na chama cha soka cha Songea vijijini
(SORUFA) ambacho kipo kisheria na kimesajiliwa kupitia msajili wa vyama vya michezo na vilabu
nchini na kina mamlaka ya kusimamia mashindano yote ambayo yanayoanzishwa vijijini na si vinginevyo.
Walisema viongozi hao ambao wanadai chama chao cha FAT kipo kisheria na kimesajiliwa kupitia kwa msajili wa vyama vya michezo na vilabu nchini na kina mamlaka ya kusimamia na kuendesha mashindano ya soka bila ya kupitia kwenye uongozi wa SORUFA , kwa kutumia uongozi wao .
Mmoja wa wadau hao wa soka,
Lezley Francis mkazi wa kijiji cha Mpitimbi “B' katika kata hiyo alipohojiwa na Mwanaperamiho blog alisema hatua iliyofikia ya viongozi wa Serikali ya kata hiyo ya kuunda chama chao cha FAT na kuendesha na kusimamia mashindano mbalimbali imekuwa ikiwashangaza baadhi ya wadau wa soka, kwani alidai SORUFA ndio chama pekee ambacho kipo kisheria na si hicho chama chao ambacho wanachodai kipo kisheria kupitia msajili wa vyama vya michezo na vilabu nchini.
Alisema kama taasisi au vyombo husika hawataliona hilo na kupiga marufuku kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wa chama hicho cha FAT ambacho wanadai kipo kisheria,
kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa mgogoro kati ya FAT na SORUFA kwani kila chama kinaweza kuja na madai kuwa wao ndio wenye mamlaka ya kusimamia na kuendesha soka katika wilaya hiyo na kupelekea kuviyumbisha vilabu wakati vikijiandaa na
mashindano ya ligi ya Daraja la Nne msimu huu.
Naye Katibu Mkuu wa FAT, John Njovu alipohojiwa na blog hii juzi kijijini hapo alisema chama chake kipo kisheria na kina uongozi kamili na kina katiba yake na kimekwisha kamilisha usajili kupitia kwa usajili wa vyama vya michezo na vilabu nchini, huku akidai wana haki ya kusimamia na kuendesha mashindano ya soka kwa mujibu wa katiba yao.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa SORUFA,
Idefonce Luoga alipohojiwa juu ya chama hicho kipya cha FAT ambacho kipo katika wilaya hiyo, alisema kwa misingi na taratibu na kanuni za Shirikisho la soka nchini (TFF) ambapo watekelezaji wake kwa ngazi ya mkoa chama cha soka cha mkoa wa Ruvuma(FARU) na kwenye wilaya hiyo ya Songea vijijini kinatambulika chama
kimoja ambacho SORUFA ndio wenye majukumu ya kikatiba ya kusimamia na kuendesha mashindano yote ya soka katika wilaya hiyo na si vinginevyo.
Hata hivyo Ofisa michezo wa halmashauri hiyo ya
Songea vijijini, Ndingo Zamngoni alipohojiwa na gazeti hili jana ofisini kwake juu ya kuwepo kwa chama kipya cha soka
katika wilaya yake ambacho kimesajiliwa kwa jina la FAT alidai hana taarifa anachokitambua ni SORUFA huku akisema kuwa kwa mujibu wa sheria kwa ngazi ya mkoa chama kimoja na wilaya kunakuwa na chama kimoja na si viwili na wanachama wao vilabu vya soka vilivyosajiliwa na visivyosajiliwa , huku akiahidi kufuatilia na kuona usajili wao ambapo alidai kwenye orodha ya vyama vilivyokuwa na usajili chama hicho cha FAT hakipo katika wilaya hiyo.
Huku, Katibu Mkuu wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma(FARU), Ahmed Challe alipohojiwa juu ya kuwepo kwa chama kipya cha soka ambacho kimesajiliwa kwa jina la
FAT ambacho kimeanza kazi ya kuendesha na kusimamia mashindano katika vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Songea alisema FARU kwa mujibu wa taratibu,
sheria na kanuni za soka ambayo iliyoundwa na Shirikisho la soka Duniani(FIFA) na kutekelezwa na Shirikisho la soka nchini(TFF) na imeshuka na kutumika kwenye ngazi ya vyama soka vya mkoa na wilaya alidai kwa kuepuka migogoro na vurugu viongozi wa chama hicho wanatakiwa wakamatwe na wafikishwe Mahakamani kwa kosa la kunyakua madaraka kinyume cha sheria za soka.
Chama hicho kipya cha FAT kwa sasa kinaendesha na kusimamia mashindano ambayo yanayoshirikisha vilabu vitano kutoka vijiji vya kata hiyo ya Mpitimbi, huku Songea
vijiji ikiwemo Tonosa Fc, Mseo Fc, Mkurumusi Fc, Stendi Fc na Muungano Fc ambapo ada ya ushiriki Sh 15,000 kwa kila kilabu na
inaendeshwa kwa mtindo wa ligi ya mzunguko mmoja , huku timu ambayo itakayokiuka taratibu, sheria na kanuni itatozwa faini ya Sh 20,000
MWISHO
Makamu Mwenyekiti wa Chama halali cha mchezo wa Soka, Wilaya ya Songea Vijijini (SORUFA) Bw. Hamdani Hamdani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni