Jumanne, 14 Julai 2015

MAFANIKIO YA YANGA NA SIMBA KUELEKEA KAGAME 2015


SOTE tumeanza kuijua kama Kagame Interclub Cup mnamo mwaka 2002, kipindi ambacha Rais wa Rwanda Paul Kagame alipoanza kuidhamini michuano hiyo inayoshirikisha vilabu bingwa kutoka Afrika Mashariki na Kati, mashindano haya yalianza mwaka 1967 na timu ya Abaluhya waliku mabingwa lakini haikuwa ikitambulika rasmi.

Mashindano Yalisimama mpaka mwaka 1974 ambapo Simba sc walipofanikiwa kuwa timu ya kwanza kuwa mabingwa kipindi ambacho michuano ilikuwa ikijulikana rasmi. 

Simba SC ndio klabu yenye mafanikio kuliko klabu yeyote kwenye mashindano hayo ikiwa imefanikiwa kuliweka kibindoni taji hilo mara 6, ikifuatiwa na mahasimu wao wa jadi vijana wa jangwani Young Africans SC iliyobeba taji hilo mara 5.

Wengi husema mafanikio ya yanga huichagiza simba sc kufanya vizuri au mafanikio ya simba sc huichagiza yanga sc kufanya vizuri, inawezekana ikawa hivyo kwani mwaka mmoja baada ya simba sc kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo mwaka uliofuata yaani 1975 Young Africans walifanikiwa kulitwaa taji hilo, maisha yaliendelea lakini historia ambayo wanajangwani hawataisahau ni ile ya kutwaa taji mara mbili mfululizo kwa miaka ya hivi karibuni yaani mwaka 2011 na 2012 huku mwaka 2012 Saidi Bahanuzi akiwa mfungaji bora wa mashindano kwa kuweka kambani goli 7, hakika ulikuwa mwanzo wa mafanikio kwa kijana huyu.

Yanga inakwenda katika mashindano hayo mwaka 2015 bila mfungaji wake bora wa mwaka 2012, nani ataibuka mfungaji bora wa mashindano mwaka huu?, je, atatoka tena yanga?
Wakati ukiendelea kuvuta picha tambua Tanzania inawakilishwa na timu tatu kama mwenyeji wa mashindano hayo, hapa nazizungumzia Azam FC, KMKM na Yanga .

Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Al Merreikh ya Sudan ambaye hata hivyo hatashiriki kutokana na kuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga imepangwa kundi A ikiwa na timu za Telecom Ya Djibouti, KMKM ya Zanzibar, Gor Mahia Ya Kenya na Khartoum ya Sudan.

Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al Ahly Shandy, LLB Ya Burundi, Elman Ya Somalia na Azam FC Ya Tanzania.

Hesabu zangu zinaniambia Azam FC baada ya kutolewa katika hatua ya robo mwaka jana, imejipanga ipasavyo mwaka huu ilikuweza kurudisha imani na thamani ya uwekezaji walioufanya, hakuna asiyefahamu Azam Complex Ulivyo uwanja wa kisasa. Michezo miwili ya kirafiki kule Tanga imetoa mwanga kwa mbali juu ya nuru iliyopo mbele ya safari.

Kule Jangwani sina shaka na kikosi chao kwani michezo minne ya kirafiki waliyocheza huku miwili ya mwisho wakiwa hawajaruhusu hata goli moja, kama sehemu ya maandalizi ya Kagame Cup imetoa mwanga pia, ushindi wa goli 3-0 dhidi ya kombaini ya polisi huku mfungaji bora wa ligi na mchezaji bora pia, Simon Msuva akiweka kambani goli moja . Ingizo jipya, Donald Ngoma aliendelea kutunisha akaunti yake ya magoli kwa kufunga bao la pili tangu ajiunge na wanajangwani.

Kama nilivyotangulia kusema, mafanikio ya Yanga huweza kutegemea yale ya Simba na kinyume chake. Baada ya Simba kuchukua mara 6, huenda Yanga nao wakatangaza ubingwa wa mara ya 6 kwani ndio nafasi adimu kwao kuamua kufanya hivyo kwani Simba hawatashiriki mwaka huu.

Chanzo: Sokatanzaniacom

Hisia kutoka Marekani na Iran


Obama amesifu mapatano hayo
Rais wa Marekani Barrack Obama amesifu makubaliano baina ya Mataifa sita makubwa yenye nguvu duniani na Iran kuhusiana na mradi wake wa kinyuklia.
Rais Obama amesema kuwa hii ndiyo nafasi ya pekee na ya hakika itakayoizuia Iran isitengeze silaha za kinyuklia.
Obama ameonya kuwa atazima jaribio lolote la bunge la Congress la Marekani kupinga kupitisha makubaliano hayo kuwa sheria.
''Nataka kutoa onyo kwa bunge la Congress la Marekani, Nitatumia kura ya turufu kuzima jaribio lolote la kuzima kutekelezwa kwa mapatano hayo ya kihistoria.''alisema Obama.
null
Rais Rouhani amesema kuwa amefurahi kuwa hatimaye vikwazo vyote vitaondolewa dhidi ya Iran
Katika hotuba ya moja kwa moja kwenye televisheni, Rais Obama amekaribisha makubaliano hayo akisema kwamba jumuiya ya kimataifa sasa itaweza kuhakikisha kuwa Iran haiwezi kutengeneza silaha hizo za nyuklia.
Amesema vikwazo vitaondolewa taratibu na Iran ni lazima itimize baadhi ya hatua na masharti kabla ya vikwazo vyote kuondolewa.
null
Kulingana na Rais Obama mapatano haya yataizuia Iran kutengeza zana za kinyuklia
Kwa upande wake Rais Rouhani amesema kuwa wamefurahi kuwa hatimaye vikwazo vyote vitaondolewa na fedha za Iran zilizofungiwa ng'ambo zitafunguliwa.
katika hotuba ndefu rais Rouhani amesema kuwa hawakuwa wanaomba washirikika wao kuwaondolea vikwazo bali walishirikiana.
'' hatukutaka kupewa msaada tuliwataka wenzetu tuwasiliane kwa heshma haki na usawa''
null
Mapatano yataruhusu wachunguzi wa kimataifa kukagua vinu vya kinyuklia vya Iran
''Tulikuwa tunatafuta vitu vinne vikuu katika mawasiliano yetu na washirika wa kimataifa nayo ni
1,utafiti wa kinyuklia uendelee,
2,kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi
3,kuondolewa vipengee tuliyodhania kuwa ni ukiukwaji wa haki zetu katika umoja wa mataifa.
null
Wawakilishi wa Iran na mataifa 6 yenye nguvu duniani baada ya kutangazwa mapatano
4, Sera kali za baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran kufutiliwa mbali
''Kwetu tumepata kila kitu tulichokuwa tumepangia na hivyo naona kuwa tumefaulu'' alisema rais huyo katika taarifa iliyopeperushwa katika runinga ya taifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ameuambia mkutano huo kwamba majadiliano hayo ya muda mrefu yamaefanikisha kukabiliana na vikwazo vyote vigumu vya miaka kumi iliyopita.
Amesisitiza kwamba Iran haijakuwa ikijaribu kuunda silaha za nyuklia.
null
Mapatano yakitangazwa
Bwana Zarif amesema yaliyomo kwenye makubaliano hayo ni magumu mno, lakini hayakuwa makubaliano tu bali ni njia ya kuelekea kutatua uhasama wa muongo uliopita.
Vikwazo vya kiuchumi ikiwemo mabilioni ya fedha mali ya Iran iliyokuwa imefungiwa katika mabenki ya nje ya nchi inatarajiwa kuachiliwa katika siku za hivi karibuni.
Vikwazo hivyo vilivyozuia Iran kuuza mafuta na gesi yake katika soko la kimatifa vilevile ilizuia usafiri wa ndege na meli taifa hilo kuingiza bidhaa ambazo sio muhimu.
Awali Katika mkutano wa waandishi habari huko Vienna mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini alisema makubaliano hayo yanadhihirisha uwajibikaji wa pamoja kwa amani na kuifanya dunia kuwa salama.
null
Waziri mkuu wa Israeli ameonya kuwa mapatano hayo ni makosa makubwa
Bi Mogherini Alisema mapatano hayo yamechangia kufikia masharti na malengo ya jamii ya kimataifa ya kuunda uhusiano.
Rais wa Iran kwa upande wake amesema kuwa ''mapatano hayo yamezuia taharuki ilikuwa bila sababu dhabiti''

Bunge la Rwanda laidhinisha muhula wa 3


Bunge la Rwanda limedhinisha awamu ya 3
Wabunge nchini Rwanda wamepitisha mswada utakaoidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba vitakavyoruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu.
Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita mamilioni ya raia nchini Rwanda wamekuwa wakitia sahihi pendekezo la kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili.
Kupitishwa kwa mswada huo sasa kunatoa fursa ya kufanyika kwa kura ya maoni ya iwapo ni haki kuruhusu uongozi wa zaidi ya mihula miwili au la.
Rais Kagame mwenyewe amesema kuwa huo utakuwa ni uamuzi wa raia wa nchi hiyo wenyewe.
null
Mamilioni ya warwanda wametia sahihi ombi la kutaka rais Kagame aendelee kutawala
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa utawala wa Rwanda unakandamiza uhuru wa kujieleza na hivyo kunyamazisha vyombo vya habari na upinzani.
Iwapo kura hiyo ya maoni itafaulu basi sheria itakuwa imefungua mlango kwa rais Paul Kagame kuwania hatamu ya tatu mwaka wa 2017.
Rais Kagame alichaguliwa kwanza katika mwaka wa 2003.

Nyuklia:Iran yakubaliana na mataifa 6 makubwa

Makubaliano yameafikiwa baina ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani
Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa makubaliano ya kihistoria yametangazwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa 6 makubwa duniani.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Iran na mataifa sita zenye nguvu duniani wanakutana kwa mara ya mwisho huko Vienna baada ya makubaliano rasmi kutatangazwa katika mkutano na waandishi habari.
null
Balozi Federica Mogherini, alipotangaza mapatano hayo
Balozi wa maswala ya kigeni wa bara Ulaya Federica Mogherini, amechapisha mwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa makubaliano kuhusiana na mradi wa kinyunklia wa Iran yameafikiwa.
Bi Mogherini amesema kuwa ni wazi mazungumzo ya kidiplomasia yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ya sera kushinda makabiliano ya kijeshi ya miongo kadhaa.
Rais wa Iran , Hassan Rouhani, amesema kuwa majadiliano hayo yamekuwa na ufanisi mkubwa
null
Makubaliano ya kihistoria yametangazwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa 6 makubwa duniani.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia aliyeko mjini Vienna anasema kuwa licha ya matokeo ya mazungumzo hayo kutojulikana inaonekana kuwa iran imekubali uchunguzi wa umoja wa mataifa kukagua mipango yake ya nyuklia.
Makabuliano hayo pia yanatarajiwa kutoa ratiba ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa Iran.
null
Rais wa Iran naye ameunga mkono mapatano hayo
Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani ametoa maelezo kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa.
Yukiya Amano amesema kuwa ''Iran imetia sahihi mpango wa kufafanua masuala yenye utata.''
Amano alisema kuwa anatarajia ukaguzi ulio kamili kwa mipango ya nyuklia nchini Iran ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameyataja kuwa ''makosa ya kihistoria''.

ROONEY, BALE?,ANGALIA ORODHA YA WACHEZAJI WA KIINGEREZA WALIOWAHI KUSAJILIWA KWA GHARAMA KUBWA ZAIDIShare on facebook

Ofa iliyokubaliwa ya Manchester City kumsajili kiungo Raheem Sterling kutoka klabu ya Liverpool imeweka rekodi mpya katika orodha ya wachezaji ghali zaidi wenye asili ya taifa la Uingereza.
Man City wamekubali kuilipa Liverpool ada ya kiasi cha paundi milioni 49 kwa ajili ya kumnasa Sterling na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi ambaye bado yupo chini ya umri wa miaka 21.
Raheem Sterling sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Gareth Bale aliyeuzwa miaka miwili iliyopita kwa ada iliyovunja rekodi ya Dunia ya paundi millioni 85.3 – akitokea Tottenham kwenda Madrid.
Andy Carrol anashika nafasi ya 3 kwa kuuzwa kiasi cha paundi millioni 35 akitokea Newcastle kwenda Liverpool.
Rio Ferdinand alinunuliwa na Manchester United akitokea Leeds United kwa Paundi milioni 30 na kuweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi kutokea kwa kipindi hicho.
Orodha kamili ya Wachezaji ghali zaidi wa Kiingereza
Paundi milioni 85.3 – Gareth Bale (Tottenham kwenda Real Madrid, 2013)
Paundi milioni 49* – Raheem Sterling (Liverpool kwenda Manchester City, 2015) * nuhamisho bado haujakamilika lakini.
Paundi Milioni 35 – Andy Carroll (Newcastle kwenda Liverpool, 2011)
Paundi milioni 30 – Rio Ferdinand (Leeds kwenda Manchester United, 2002)
Paundi milioni 27 – Luke Shaw (Southampton kwenda Manchester United, 2015)
Paundi milioni 27 – Wayne Rooney (Everton kwenda Manchester United, 2004)
Paundi milioni 26 – James Milner (Aston Villa kwenda Manchester City, 2010)


        SHEIN: MAGUFULI NDIYE KIBOKO YAO

Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohammed Shein akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema uteuzi wa mgombea wa CCM katika nafasi ya rais wa Jamhuri ya Muungano katika uchaguzi mkuu, Dk John Magufuli ndio chaguo sahihi la kupambana na upinzani na kuleta ushindi katika CCM na kushika dola.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Zanzibar kutoka Dodoma, Dk Shein alimtaja Magufuli kama kiongozi hodari muaminifu mwenye shauku kubwa ya kuleta maendeleo ya nchi yake.
Dk Shein katika mkutano mkuu uliomalizika Dodoma hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imemwidhinisha kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM tayari kupambana na chama kikuu cha CUF.
Alisema, Magufuli katika nyadhifa mbalimbali alizoshika ameonesha uhodari wa kuchapa kazi na uzalendo pamoja na kusimamia majukumu yake pamoja na walio chini yake. Alifahamisha kwamba ndiyo kigezo sahihi cha kupambana na wapinzani na kuleta maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
‘’Mimi namfahamu vizuri sana Magufuli nimefanya kazi naye katika kipindi cha miaka 9 katika baraza la mawaziri nikiwa makamu wa rais......ni mchapa kazi hodari, mwadilifu mwenye mapenzi makubwa na wananchi wake,’’alisema.
Kwa mfano alisema katika Wizara zote alizopata kufanya kazi alionesha uwezo wa ubunifu wa kuleta maendeleo akizitaja Wizara ya Uvuvi pamoja na Ujenzi.
Aidha alimpongeza kwa kumteua Samia Suluhun Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kuwa mgombea mwenza huku Chama Cha Mapinduzi kikiweka rekodi ya kuwa na mgombea mwenza mwanamke.
Alisema Samia ameonesha uwezo wa kazi katika nafasi mbalimbali alizopata kuzishika tangu akiwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi Muungano.
Alifahamisha kwamba Demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi imeimarika kwa kiwango kikubwa ambapo nafasi za wanachama mbalimbali kugombea nafasi za juu za uongozi ni kubwa sana ikiwemo wanawake.
Kwa mfano, alisema Chama Cha Mapinduzi kimeweka historia kubwa ya kuteua wanawake wawili kuingia katika hatua ya mwisho ya uteuzi wa tatu bora. ‘’Hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi demokrasia yake katika makundi mbalimbali imekuwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo wanawake kushirikishwa katika mchakato wa hatua za mwisho na kushika nafasi ya mgombea mwenza,’’ alisema.
Alipoulizwa kuhusu wingi wa wagombea wa nafasi ya juu ya urais, alisema demokrasia katika Chama Cha Mapinduzi imepanuka kwa kiwango kikubwa tofauti na vyama vyengine vya siasa.
Alisema katika mchakato wa nafasi ya urais jumla ya wanachama wa CCM 42 walijitokeza kuwania nafasi hiyo tofauti na miaka ya 2000 ambapo walijitokeza wanachama 17. ‘’Chama Cha Mapinduzi kinajengwa kwa nguvu ya msingi mmoja mkubwa ambao ni demokrasia iliyopevuka inayotoa makundi mbalimbali ya wanachama kuwania nafasi za juu za uongozi,’’alisema.
Akisoma risala ya wananchi wa mikoa sita kichama, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM Zanzibar), Shaka Hamdu alisema wamefurahishwa na maamuzi ya vikao vya chama kuwateuwa wagombea wa nafasi za juu za urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.
Shaka alisema wanachama wa CCM Zanzibar wanaunga mkono uteuzi huo wa majina ya viongozi hao ambao watapeperusha bendera ya chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kukileta ushindi chama.
‘’Wanachama wa mikoa sita matumaini yao makubwa kwamba wagombea wa nafasi za urais kuanzia John Magufuli nafasi ya urais wa Muungano pamoja na Dk Ali Mohamed Shein kwa nafasi ya urais wa Zanzibar kwamba ni uteuzi sahihi wa wagombea wenye sifa watakaokiletea chama ushindi,’’alisema.
Mamia ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla wamejitokeza katika mapokezi ya mgombea wa urais wa Zanzibar kuanzia uwanja wa ndege wa Abeid Amaan Karume hadi katika makao makuu ya CCM Kisiwandui.

TMT YAZIDI KUNOGA, WAWILI TENA WATOLEWA!

Baadhi ya washiriki wa shindano la kuibua vipaji vya kuigiza la TMT wakiwa kwenye jua la utosi.
Majaji wa TMT kutoka kushoto ni Richie, Monalisa pamoja na Roy.
Washiriki waliotoka jana kwenye shindano hilo, Rosemary Kivuyo wa Dar pamoja na Lameck Paul wa Mbeya.
Watangazaji wa TMT, Lulu pamoja na Mboto wakitangaza.
Mtangazaji wa TMT, Mboto (katikati) akiwa na wahudhuriaji waliojitokeza kuangalia shindano hilo.
Baadhi ya washiriki wa TMT mwaka huu wakisubiri kuitwa kwenye jua la utosi.
Wahudhuriaji katika shindano la TMT wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Mwalimu wa washiriki, Julieth Samson (Kemi) akifuatilia washiriki.
Jaji Mboto akiongoza shindano hilo.
(KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)