Nyuklia:Iran yakubaliana na mataifa 6 makubwa
Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa makubaliano ya kihistoria yametangazwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa 6 makubwa duniani.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Iran na mataifa sita zenye nguvu duniani wanakutana kwa mara ya mwisho huko Vienna baada ya makubaliano rasmi kutatangazwa katika mkutano na waandishi habari.
Balozi wa maswala ya kigeni wa bara Ulaya Federica Mogherini, amechapisha mwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa makubaliano kuhusiana na mradi wa kinyunklia wa Iran yameafikiwa.
Bi Mogherini amesema kuwa ni wazi mazungumzo ya kidiplomasia yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ya sera kushinda makabiliano ya kijeshi ya miongo kadhaa.
Rais wa Iran , Hassan Rouhani, amesema kuwa majadiliano hayo yamekuwa na ufanisi mkubwa
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia aliyeko mjini Vienna anasema kuwa licha ya matokeo ya mazungumzo hayo kutojulikana inaonekana kuwa iran imekubali uchunguzi wa umoja wa mataifa kukagua mipango yake ya nyuklia.
Makabuliano hayo pia yanatarajiwa kutoa ratiba ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa Iran.
Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani ametoa maelezo kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa.
Yukiya Amano amesema kuwa ''Iran imetia sahihi mpango wa kufafanua masuala yenye utata.''
Amano alisema kuwa anatarajia ukaguzi ulio kamili kwa mipango ya nyuklia nchini Iran ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameyataja kuwa ''makosa ya kihistoria''.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni