Jumapili, 21 Juni 2015

UTAFITI:WATOTO WAONGO NDIYO WENYE AKILI ZAIDI KULIKO WASIODANGANYA

 

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.

Watafiti katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma ya karatasi zao za kujibia.

Wale waliodanganya kuhusu kile walichofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.

Mmoja wa watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uongo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni