Alhamisi, 9 Julai 2015





Image result for breaking news

AMANA MBABAZI AZUIWA NA POLISI UGANDA

Waziri mkuu wa zamani Uganda Amama Mbabazi
Vyombo vya habari Uganda vinaarifu kwamba Kizza Besigye aliyekuwa mkuu wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) pia amekamatwa.
Inaarifiwa kwamba Polisi inamhamisha Amama Mbabazi kutoka Njeru eneo la kati mwa Uganda, na kumpeleka katika mji mkuu Kampala.
Haijulikani wazi ni kwanini anazuiwa na polisi.
Mbabazi amewahi kuonywa dhidi ya kufanya mikutanop ya umma kushinikiza azma yake ya kuwania urais.
Msaidizi wa bwana Mbabazi Justin Nkangi pamoja na wakili wake wamethibitisha kukamatwa kwa Mbabazi.
null
Rais Museveni alimuachisha kazi Mbabazi kama waziri mkuu 2014
Kwa muda mrefu Amama Mbabazi amekuwa mshirika wa karibu sana na Rais Yoweri Museveni hadi alipofutwa kazi mwaka jana kama waziri mkuu.
Wadadisi wameelezea tofauti zake na rais Museveni kutokana na Nia yake ya kuwania Urais, ambapo atakabiliana na rais Museveni na mkuu wa Upinzani Dr. Kizza Besigye.
Kabla ya kushikilia nafasi ya Waziri mkuu, Amama Mbabazi aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa Uganda. Pia amekuwa mbunge wa Kinkiizi magharibi wilaya ya Kanungu.
Amehudumu pia kama katibu mkuu wa chama tawala cha Uganda NRM. Mke wake pia anashikia wadhifa wa kiongozi wa kundi la wanawake katika chama hicho cha NRM. (Via BBC)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni