MKWASA ATAKA MSAADA WA SERIKALI

KOCHA wa timu ya Taifa Stars, Charles Mkwasa ametoa mwito kwa Serikali kuwa karibu na timu hiyo kwa kutenga bajeti angalau kidogo kuisaidia ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wao dhidi ya Uganda, Mkwasa alisema katika nchi yoyote duniani timu za taifa haziwezi kuendelea bila kuwepo mkono wa Serikali.
“Bila uwezeshwaji wa Serikali hatuwezi kupata timu bora na nzuri, ni muhimu ikaangalia na huku kuona kama wanaweza kuunga mkono ili kutimiza malengo ya kufanya vizuri,”alisema.
Aidha, alizungumzia kuhusu mikakati ijayo kuwa wataendelea kuchagua wachezaji kwenye michuano ya Kagame itakayofanyika kuanzia Julai 18, mwaka huu.
Alisema baada ya michuano hiyo ataita kikosi kwa ajili ya mazoezi, ambapo baadaye atataja kikosi ambacho kitajiandaa na michuano ya Afrika dhidi ya Nigeria.
Wakati huo huo, Mkwasa hakusita kupongeza mashabiki wa soka Tanzania kwa kuamua kuweka silaha chini na kuwaunga mkono katika mchezo dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini humo.
Katika mchezo huo wa kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya Chan, Taifa Stars ililazimishwa sare ya bao 1-1 na kutolewa kwenye mashindano hayo baada ya awali katika mchezo wa nyumbani kufungwa mabao 3-0.
Aliwashukuru pia wachezaji kwa kucheza kizalendo na kujituma uwanjani na ingawa hakufanikiwa.
“Wachezaji walijituma sana na kucheza kwa nidhamu, tulipanga ndani ya dakika 15 tuwe tumepata goli, tukatumia mfumo wa kushambulia ingawa kuliko na changamoto nyingi,”alisema.
Alisema Uganda haikuwa timu ya kuwatoa kulingana na mchezo waliouonyesha katika mchezo wa marudiano, kwani baada ya kuwabana waliona njia pekee itakayowasaidia ni kucheza rafu ambapo walifanikiwa.
Alisema walipoteza nafasi nyingi katika mchezo huo, sasa
kuomba kupewa muda zaidi wa kujiandaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni