NIONAVYO
MIMI: UHAI WA UDONGO NI RAHISI KUHARIBIKA PIA UCHOMAJI OVYO WA MASHANBA YETU
PINDI TUNAPOANDAA MASHAMBA
Ndugu zangu wakulima naomba
tuelimike, tubadilike katika harakati za uandaaji wetu mashamba pindi
tunapoanza uandaaji wa mashamba yetu ya kilimo. Ndugu wakulima mabadiliko
yenyewe ni haya yafuatayo:
Kutokutumia moto wakati wa
kusafisha na kupanda mashamba yetu ya kilimo moto ni chanzo kikubwa cha
uharibifu. Uharibifu unaua vitu vyenye uhai vinavyolisha vidudu vyote viishivyo
ardhini. Pia si hivyo tu moto unaua na kufukuza toka ardhini wanyama, wadudu,
viumbe vidogo na mimea yenye manufaa.
Mfano, moto unaunguza shamba lako
kila mwaka sehemu hiyo hiyo unafukuza kabisa aina fulani za mimea na wanyama.
Hubakiza mimea na viumbe vinavyoweza kuvumilia. Ndugu mkulima, kuna viumbe hai
vingine vingi vinavyoishi na kukaa katika udongo wa juu. Viumbe hivi ni wanyama,
wadudu, minyoo, uyoga, vihadubini, mchwa n.k. Ndugu mkulima kila kinachoishi
ndani ya ardhi au juu ya ardhi hufa na kutoa mboji. Vyote hivi vina manufaa
makubwa katika kilimo. Ndiyo maana unashauliwa kuwa wakati unapomaliza msimu wa
masika pia wakati unapomaliza kuvuna mahindi au mazao mengine unashauliwa
kutokutumia moto wakati unapojiandaa na msimu mwingine.
Ndugu mkulima, viumbe vingi vinaishi
ardhini ambamo vinakula na kutupa uchafu wao. Vinachimba udongo,
vinausafirisha, kwa hiyo maisha ya udongo ni ya muhimu kwa rutuba ya ardhi. Na
kuua maisha haya kwa njia mbaya za kilimo ni kuhatarisha maisha ya baadaye ya
udongo. Hivi ndugu zangu wakulima viumbe hai ndivyo vinavyotegeneza mboji
ambayo ni sehemu muhimu kwa maisha ya udongo na kwa kulisha mimea. Mboji
hupatikana baada ya takataka zitokanazo na mimea na wanyama kutumiwa na viumbe
vyote vinavyoishi ardhini, isipokuwa mizizi.
Ndugu mkulima ngoja tuangalie
kwanza kabisa viumbe hai gani huishi ardhini. Mchwa ndio walaji wakubwa wa miti.
Huikatakata miti katika sehemu ndogo ndogo na laini na kurahisisha kitendo cha
kuzibadilisha ziwe mboji huhamisha udongo na kuuchanganya na mabaki ya miti na
vitu vingine hai.
Visisimizi nao hufanya kazi kama
hiyo. Hawa hupendelea vitu vilivyo bado vibichi kama majani, mbegu, mabaki
mabichi, mizoga, uyoga na majani madogo madogo laini (moss). Tunaweza kusema
kuwa mchwa na sisimizi ni muhimu sana katika mfumo huu wote wa chakula
unaotengeneza mboji inayoipa ardhi sifa zake za kilimo.
Wadudu, mafunza na konokono kuna
mamiaya aina ya mafunza na waishio ndani ya udongo. Wengine wanaonekana kwa macho
na wengine ni wadogo sana hawaonekani kabisa kwa macho walio wengi kati ya
viumbe hao wanaishi kwa mabaki ya mimea, viumbe
wengine uyoga na majani madogo laini, vinyesi, vyoo vinafanya mboji.
Ndugu mkulima, ifahamike kwamba
mizizi na viumbe hivi inabidi kuishi pamoja. Mizizi inatafuta sehemu ambazo
viumbe hivi vimekwisha geuza vitu vyenye asili ya uhai kuwa mboji viumbe hivi
vinafanya kazi karibu na mizizi kwa sababu mizizi inazitupa takataka karibu
katika udongo.
Viumbe vyote vilivyo ardhini
vinashirikiana katika kazi hii ya kubadilisha vitu kwa ajili na faida ya mimea.
Kwa hiyo mkulima anatakiwa kujifunza kuvisaidia kwa njia zote anazoweza
kuvifanya viumbe hivyo viishi. Kuangamia kwa viumbe hivi kunaweza kufanya ardhi
isiwe na rutuba.
Imeandaliwa na Mkandidati Robart Elias
Plasido Peramiho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni