SUALA LA WAHAMIAJI BARANI ULAYA BADO KITENDAWILI
Nchi za Ulaya zimeshindwa kuafikiana kuhusu namna ya kuwashughulikia maelfu ya watu wanaoingia barani Ulaya kupitia Italia na Ugiriki kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Nchi hizo mbili zimezitaka nchi za Umoja wa Ulaya, EU kusaidiana kubeba majukumu ya kuwahudumia wahamiaji lakini mataifa ya mashariki kama Poland na Hungary zimepinga mgawo wa lazima wa kuwahudumia watu hao, wakati ambapo Ufaransa na Ujerumani zikitaka wale wanaobainika kuwa wahamiaji wa kiuchumi kurejeshwa katika nchi zao za asili.
Mwandishi wa habari wa BBC katika mkutano huo amesema makubaliano huenda yakatolewa na viongozi wa EU wiki ijayo lakini mgogoro huo unadhoofisha umoja wa Ulaya. Mapema, polisi wa Italia walivunja kambi inayowahifadhi wahamiaji kutoka Afrika ambao wamenyiwa idhini ya kuingia Ufaransa.

Wahamiaji wakisubiri kupanda meli katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia kuhamishiwa Porto Empedode, Sicilia Aprili 17,2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni