Jumatatu, 15 Juni 2015


SIMANZI MAFINGA: WATU 23 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 34 WAMEJERUHIWA KWA AJALI YA BASI


Watu 23 wamepoteza maisha na wengine 34 wamejeruhiwa katika ajali ya bus iliyotokea juzi usiku katika eneo la kinyanambo A wilayani Mufindi barabara kuu ya Iringa -Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Pudenciana Protas alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya 19:45 usiku katika eneo la Kinyanambo wilayani hapo.

Kamanda Protas alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari kampuni ya Another G express yenye namba za usajiri T.927 CEF na gari ya kampuni ya Bravo Logistic (T) limited yenye namba za T.916 AQM lenye trela namba T.595.



Mkuu wa Wilaya wa Mufindi Mboni Mhita akimjulia hali mmoja wa majeruhi wa ajali katika hospitali ya wilaya ya mufindi mjini mafinga

Waliofariki dunia na kutambuliwa mpaka sasa ni Lukas Pascal, Brasto Samila, Dickson Luvanda, Albert Silla, Rogers Mdoe, Eva Mbalinga, Hadija Mkoi, Clemence Mtati, Mohamed Kalika, Kastoli Mwakyamba, Damian Myala na Sillo Nziku.

Waliojeruhiwa ni Majoline Lupembe (23) mkazi wa Iringa, Veronica Simba (20) mkazi wa Tabora, Shadia Ally (24) mkazi wa Iringa, Mariam Mbise (23) mkazi wa Mafinga, Anita Makwela (24) mkazi wa Kilolo, Benita Sagala (18) mkazi wa
Njombe, Bertha Mkoi (27), Rahel Mavika (18) mkazi wa Mufindi, Selina Fulgence (23) mkazi wa Kigoma na Maria Mwenda (17) mkazi wa Mafinga.

Ndugu na jamaa wajitokeza katika mochwari ya Mafinga kutambua miili ya ndugu zao waliokufa katika ajali

Wengine ni Ndipako Mbilinyi (23) mkazi wa Njombe, Alexander Mkakazii (28) mkazi wa Mafinga, Meshack Kibiki (44) mkazi wa Mafinga, Simon Jumbe (22) mkazi wa Singida, Jerry Lutego (36) mkazi wa Mafinga, Enock Kanyika (18)
mkazi wa Mafinga, Deogratius Kayombo (21) mkazi wa Mafinga na Yusuph Lulanda (22) mkazi wa Njombe.


Wengineo ni Petro Mwalongo (21) mkazi wa Njombe, Paulo Chane (21) mkazi wa Kilolo, Kenned Msemwa (28) mkazi wa Njombe, Mode Shiraz (21) mkazi wa Singida, Emmanuel Antony (21) mkazi wa Mwanza, Godfrey Kanyika (39) mkazi wa Mafinga, Boniface Bosha (20) mkazi wa Sumbawanga, Ambiana Meshack (35) mkazi wa Njombe, Martha Kanyika (30) mkazi wa Mafinga, Merina Tonga (miezi miwili), Yusuph Luhamba (34) mkazi wa Mafinga na wanaume wawili na wanawake wawili ambao hawajaweza kutambulika majina yao kutokana na hali zao kuwa mbaya.



(Kwa hisani ya Simbaya Blog)






--

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni