BAADA YA MHOLANZI MART NOOIJ NA BENCHI LAKE KUTIMULIWA, RASMI MKWASA NA MATOLA WAKABIDHIWA KIKOSI CHA STARS
CHARLES BONIFACE MKWASA 'MASTER' ameteuliwa Kocha Mkuu wa muda wa Taifa Stars baada ya benchi lazima la ufundi la timu hiyo kutimuliwa
Kocha Msaidizi wa Yanga,Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania kwa muda akisaidiwa na Selemani Matola.
Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya Yanga anachukua nafasi ya Mart Nooij aliyetimuliwa pamoja na benchi lake lote la ufundi baada ya Taifa stars kuchapwa goli 3 - 0 dhidi ya Uganda "The cranes".
Mara moja Mkwasa na Matola wataipokea timu hiyo kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Waganda hao.
SULEIMAN MATOLA atamsaidia Mkwasa kukinoa kikosi cha Stars kwa muda
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni